|

BARNABA KWENDA UFARANSA KUREKODI 'TUACHANE KWA WEMA' NA FALLY IPUPAMSANII mahiri katika miondoko ya muziki wa Bongo Flava Barnara,anataraia kuondoka nchini Machi 28, mwaka huu kuelekea nchini Ufaransakwa ajili ya kurekodi kibao chake kipya kiitwacho 'Tuachane kwa Wema,ambacho atamshirikisha mwanamuziki nyota wa muziki wa Dansi FallyIpupa. Akizungumza na mtandao huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com,Barnaba, alisema kuwa maandalizi yote ya safari hiyo tayariyamekamilika na tayari amekwishapewa 'Apointment' na moja ya Studio zanchini humo tarehe ya kufika na kurekodi wimbo wake huo. Aidha Barnabaalisema kuwa wimbo huo utakuwa ni miongoni mwa nyimbo zakezitakazokuwamo katika albam yake mpya itakayokuwa na jumla ya nyimbo10, ambayo inatarajia kukamilika mwezi wa sita mwaka huu. ''Unajuakatika ndoto zangu za kimuziki nimekuwa na ndoto siku nyingi yakurekodi na mastaa wa ukweli Duniani, na Fally ni mwanzo tu kwani wapowengine ambao tayari nimeshawasiliana nao pande za mamtoni ambaotayarikama watatu wamekwisha nithitishia kunipa 'shavu' katika miongonimwa nyimbo zangu kadhaa ambazo nyingine zitakuwa ni katika albam yanguijayo baadaya hii. Hata Fally pia alikuwa akitamani kurekodi na mimitangu nilipo mpagawisha katika moja ya shoo yake alipokuja nchini nakuipenda sauti yangu, kwa hiyo naye nipi ni nafasi yake pekee aliyokuwaakiitamani ambayo amefanikiwa'' alisema Barnaba Barnaba alisema kuwambali na wimbo huo lakini pia anatarajia kurekodi video ya wimbo huo,awapo nchini humo iwapo atafanikiwa kumaliza ndani ya muda uliopangwana mwandaaji wake. Alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazokuwa katika albamhiyo kuwa ni pamoja na Gubegube, Sidhani Kama na Roho si Moyo, ambazozote tayari zimekwisharekodiwa katika Studio za THT.

Posted by Bongo Flavor on 1:58 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added