|

RAY ANASWA KABURINI KWA KANUMBA
KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alinaswa mchana kweupe kwenye kaburi la aliyekuwa swahiba wake, marehemu Steven Kanumba lililopo Kinondoni jijini Dar, Ijumaa Wikienda limeinasa.

Siku ya tukio
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitutonya kuwa siku hiyo Ray alifika makaburini hapo na kwenda moja kwa moja mahali lilipo kaburi hilo kisha kuliinamia kwa dakika kadhaa huku akionekana mwenye jambo moyoni.
“Sisi tulikwenda pale kulifanyia usafi kaburi la ndugu yetu. Mara tukamuona Ray akiingia na kwenda kwenye kaburi la Kanumba, ni kama mtu aliyekuwa akimuombea dua hivi…,” alisema mtoa habari huyo na kuongeza:
“Ninachojua mimi mpaka Kanumba anafariki, walikuwa kwenye bifu na sikumbuki kama liliisha ‘so’ huenda alifika pale kwa nia ya kumuomba msamaha ili huko alipo amsamehe.”

Rafiki yake atoboa
Hata hivyo kabla ya kuzipata taarifa hizo, juzikati rafiki wa Ray ambaye naye aliomba hifadhi ya jina lake aliliambia gazeti hili kuwa msanii huyo amekuwa akiumia sana kila anapokumbuka bifu lake na marehemu.
“Jamaa kila anapokumbuka kuwa Kanumba kaondoka wakiwa bado hawajakutana na kusawazisha mambo, anakosa raha sana.
“Alisema ipo siku atakwenda kuongea na marehemu pale kaburini ili huko aliko ajue anaumia kwa hali hiyo,” alidai mtoa habari huyo.

Ray anasemaje?
Katika kujua ukweli wa tukio hili, mwandishi wetu alimtafuta Ray kupitia simu yake ya mkononi na alipopatikana alikiri kufika kwenye kaburi la swahiba wake huyo.
“Ni kweli nilikwenda pale kwenye kaburi la Kanumba kama ambavyo ndugu, jamaa na marafiki wamekuwa wakienda,” alisema Ray kwa kifupi.
Alipobananishwa kuwa inadaiwa kilichompeleka ni kwenda kuomba msamaha kwa yale yaliyotokea kati yao enzi za uhai wake, Ray alisema:
“Nilishaongelea mara kadhaa ishu ya tofauti yangu na marehemu kwamba mpaka anafariki dunia tulikuwa tupo sawa.”

Tujikumbushe
Enzi za uhai wake, Kanumba na Ray walikuwa kwenye bifu lakini baadaye ikadaiwa waliwasiliana kwa simu na kuondoa tofauti zao licha ya kwamba hawakuweza kukutana uso kwa uso mpaka umauti ulipomkuta.

Posted by Unknown on 11:09 PM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added