|

Danny Mrwanda Aigeuka Yanga, Ahamia Simba

 MAKAMU Mwenyekiti wa mabingwa wa Tanzania Simba SC Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ amesema club hiyo imekamilisha usajili wao kwa kukinasa kifaa kimoja kikali ambacho Yanga walikuwa wanakiwania.
Ingawa Kaburu hakutaka kutaja jina la mchezaji huyo, lakini uchunguzi wa BIN ZUBEIRY umebaini kwamba, mchezaji mwenyewe ni mshambuliaji wa Dong Tam Long An ya Vietnam, Danny Davis Mrwanda ambaye kweli Yanga walikuwa wanamtaka wakashindwana.
BIN ZUBEIRY inajua Mrwanda aliyewahi kuchezea Simba kabla ya kwenda ughaibuni, atasaini Simba SC wakati wowote kwa sababu mazungumzo baina ya pande hizo mbili yanaendelea vizuri.
Mkataba ambao atasaini Mrwanda ni ambao utamruhusu kuondoka wakati wowote atakapopata timu nje ya Tanzania.
Pamoja na ishu ya Mrwanda, Kaburu alisema kwamba mchezaji anayefunga usajili wa Simba ni beki wa kati wa kigeni, ambaye bado wanafuatilia uwezo wake ili kujiridhisha.

Lakini Kaburu amesema mahitaji yote ya Simba yametimia, kwa kusajili winga Kiggi Makassy, washambuliaji Abdallah Juma, Mrwanda, viungo Ibrahim Jeba, Patrick  
Mbivayanga, Salim Kinje, Mussa Mudde, beki wa kushoto, Paul Ngalema na kupandisha wachezaji watatu wa U-20.
Aidha, Kaburu alisema ili kuboresha zaidi kikosi, wanafikiria kusajili beki wa kulia kwa sababu Nassor Masoud ‘Chollo’ ni majeruhi wa muda mrefu na kuna uwezekano bahati ikamuangukia beki wa timu hiyo aliyekuwa akicheza kwa mkopo Villa Squad, Haruna Shamte.
Kwenye sentensi nyingine ni kwamba Kiggi Makassy ameripoti rasmi kazini, kwa mwajiri wake mpya Simba SC na kuanza mazoezi leo asubuhi. “Kiggi ameanza mazoezi rasmi leo,”alisema Kaburu kuhusu kiungo huyo waliyemuiba kwa watani wao wa jadi, Yanga SC.  (Stori yote imeandikwa na Bin Zubery wa

Posted by Unknown on 3:58 AM. Filed under , , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added