|

YOUNG D: NI KWELI NILIPATA AJALI WAKATI NATOKA KWENYE SHOW YA SIMBA.


Rapper Young Dar es salaam amekiri kwamba alipata ajali usiku wa jumapili wakati akitoka kufanya show ya club ya Simba kusherehekea ubingwa wake wa ligi kuu Dar Live Mbagala Dar es salaam.

D amesema hiyo ndio sababu kubwa iliyomfanya hata ashindwe kuperform kwenye show ya Rachel wa THT Maisha Club.

Chanzo cha ajali ni dereva Taxi akiwa kwenye spidi kubwa kujaribu kumkwepa mvuka barabara hivyo ikabidi afanye maamuzi ya ghafla na kugonga nguzo na kuingia mtaroni kitendo ambacho kilimfanya Young D apoteze fahamu hapohapo kwenye eneo la ajali, alipelekwa hospitali kuanzia hiyo saa tano usiku na kuruhusiwa kutoka saa nane usiku huo huo.

Hata hivyo mbali na hiyo ajali, D amekubali kwamba amelipwa zaidi ya shilingi milioni moja kwa kuwa msanii pekee wa bongofleva kualikwa kwenye show hiyo ya Simba ambayo mashabiki wake waliutumia wimbo wake wa dada anaolewa na kuuita Yanga anaolewa baada ya kuishinda Yanga kwenye fainali, hiyo ndio sababu kubwa iliyofanya D aalikwe kuperform.

Posted by Unknown on 12:13 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added