|

Alichosema Nazizi kuhusu wanao mponda Prezzo kwenda Big Brother


Baada ya Prezzo kuwa topic kubwa kwenye mitandao ya kijamii ya twitter na facebook hasa kwa baadhi ya wakenya ambao wamekua wakiponda yeye kwenda big brother akiwemo msanii Jaguar, mshkaji wa karibu wa Prezzo, mkali Naziz wa Necessary noise amekubali kuelezea wengi wasichofahamu kuhusu Prezzo.
Amesema “sijaangalia Big Brother lakini nimekua nikiona watu wanamuongelea kwenye twitter na facebook, lakini kuna sababu zilizofanya watu waliokwenda Big Brother kuchaguliwa, lazima walijua Prezzo ni mbishi ni mtu ambae ni sahihi akiwepo sehemu kama hiyo”
kwenye sentensi nyingine Naziz kasema “Prezzo ni mbishi ni rafiki yangu namjua japo sijaangalia Big Brother najua lazima ubishi utakuepo na huwa hasikilizi na uhakika kwamba wasichana watakua wanamchukia kinoma au watakua wanampenda, vilevile ni Mkenya na inabidi tumsupport”
Kwa kumalizia Naziz amesema “watu wanamchukulia yule Prezzo kwa Big Brother kwa kile wanachokisoma kwenye Media kuhusu yeye lakini Media na Prezzo hawajawa kwenye uhusiano mzuri, yani hata kama Prezzo anajaribu kufanya nini Media Kenya bado ilikua inamdiss wakati wote kwa sababu ni CMB na anajiona ana pesa lakini ni mtu tofauti wakimpa nafasi watamjua vizuri, sitazami Bog Brother lakini namuunga mkono”
Hiyo ni kauli ya Naaziz ambae sasa hivi yuko Bongo kwa ajili ya kuperform leo Zonghua Garden Dar es salaam kwenye Reggae show ambayo itakua na vichwa vikali vingine kama washindi wa KTMA 2012, Warriors from the East pamoja na 20%.
Mpaka sasa Naaziz ni mmoja kati ya wakenya wachache walioperfom Tanzania mara nyingi, alianza kuperform bongo miaka 15 iliyopita.

Posted by Unknown on 2:44 AM. Filed under , . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added