|

MR NICE ASEMA ALIETOA HIZI TAARIFA NI MNAFIKI!


Staa wa long time kwenye Bongofleva Lucas Mkenda au Mr Nice amekanusha taarifa zilizosambazwa dhidi yake kwamba alishushwa kwenye stage na mashabiki baada ya kutopendezwa na show aliyoifanya huko Zambia siku kadhaa zilizopita, huku sababu kubwa zikitajwa kuwa ni kuimbia CD wakati mashabiki hao walitegemea angeimba LIVE na Band.
Nice amesema aliesambaza hizo habari ni mnafiki na kuamplfy zaidi kwamba “unajua watu wengi wanapenda kuharibia watu wengine tu kwa kuongea uongo, kwani ni wasanii wangapi wamarekani wanatoka huko na kuja kufanya show za Cd hapa? kama kweli mashabiki hawakupenda show yangu ya Zambia basi uwanja usingejaa”
Staa huyu wa single mpya iitwayo Tabia gani amesema “Kuna nyimbo nyingine huwezi kupiga live, na pia kuna show nyingine tunafanya bila band kwa sababu ya mapatano ya promota kwa sababu live band ni bei kubwa zaidi, pia inategemea na aina ya watu utakaokwenda kuwaimbia”.
Habari kwa Hisani ya : http://millardayo.com/

Posted by Unknown on 1:55 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added