|

MASTAA WANAO TUMIA MADAWA YA KULEVYA WATAJWA


Na Musa Mateja

Kifo cha malkia wa muziki wa Pop, RnB na Soul wa Marekani, Whitney Elizabeth Houston kilichochangiwa na matumizi ya madawa ya kulevya, kimeibua mapya ambapo listi ya mastaa wa Kibongo wanaodaiwa kutumia madawa hayo yakiwemo ‘unga’, bangi, mirungi na mengine imetajwa, Risasi Jumamosi lina ripoti kamili.

Habari za chini kwa chini zinadai kuwa kwa sasa mastaa kibao wanatumia madawa ya kulevya huku majina makubwa kama Msafiri Sayai ‘Diouf’, Albert Mangwair, Langa Kileo, Rehema Chalamila ‘Ray C’, Waziri Makuto ‘Lord Eyez’, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, Aisha Mbegu ‘Madinda’, Khaleed Mohamed ‘TID’, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’, Abas Kinzasa ‘20%’, David Nyika ‘Daz Baba’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Happiness Thadei ‘Sister P’ na Rose Ndauka yakitajwa.

“Chondechonde, tuungane kuwakanya mastaa wetu kwani wataondoka bado tukiwa tunawahitaji kama alivyoondoka Whitney na miaka 48. Wazazi, ndugu, jamaa na marafiki tulindane na janga hili kwani litawamaliza vijana wetu ambao ndiyo nguvu kazi,” ilisomeka barua pepe iliyotumwa kwenye gazeti hili mwanzoni mwa wiki hii.

Baada ya kuinyaka listi hiyo, timu yetu ilizungumza na baadhi ya mastaa hao ambapo walikuwa na haya ya kusema.

Fid Q: Sijawahi kuvuta unga katika maisha yangu ila niliwahi kufanya kazi na shirika binafsi linaloitwa Rafiki Family lililokuwa likihamasisha watumiaji wa madawa ya kulevya waache na nilifanikiwa kutibu wawili nikiwa kama mwanamuziki maarufu.

TID: Hayo ni madai tu, sijihusishi kwa namna yoyote na madawa ya kulevya, watu wanasema tu kwa sababu mimi ni staa, ninayependa maendeleo na familia yangu, isitoshe siku zote mtafutaji hakosi kashfa.

Posted by Bongo Flavor on 10:46 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added