|

KUFA KWA MUZIKI WA BONGO KUNACHANGIWA NA BAADHI YA WASANII WAKUBWA WA HAPA NYUMBANI.

Tulitegemea kwa wasanii wakubwa kama Ambwene yesaya ama A.Y kama anavyofaamika kwa mashabiki wengi wa muziki, angekuwa ni mfano wa kuigwa na wanamuziki chipukizi hapa nchini,ila ila baadala yake ameonekana kutokuwa na discipline na kikwazo kikubwa cha kukua kwa muziki wa reggae na ragga hapa nchini.

Sisi kama Jahson na susu hatuwezi kujifunza lolote kutoka kwa msanii huyo (A.Y) kwa sababu amekuwa ni mtu alionyesha utovu wa nidhamu ya hali ya juu mara kadha wa kadha mfano.

Wengi tunamjua A.Y kama msanii wa hip hop lakini mwaka 2010 aliwai kushindania tunzo ya mwanamuziki bora wa reggae na hatimaye kupata tunzo hiyo na kuichukua kwa mbwebwe zote na Pia mwaka huu 2012 amewekwa kwenye category ya ragga na nina imani atapata tu tunzo hiyo kutokana ma madhaifu yaliyopo katika uandaaji wa tunzo hizo za Kilimanjaro music award.

Bushoke alikuwa mfano mzuri sana wa kuigwa alipopewa tunzo ambayo hakustahili na kuikataa je A.Y kwa nini alikubali tunzo hiyo? Na ki ukweli haikumstahili

Ki ukweli wasanii kama A.Y wanatuvunja moyo sana sisi wasanii ambao tunaofanya muziki huo pamoja na mashabiki wa muziki huo wa reggae na ragga na kwa taharifa yake tu bwana AY asijidanganye kwa wingi ama uchache wa kura hizo anazopata katika kinyang’anyilo hicho ,asidhani kama anapigiwa na mashabiki wa Reggae na ragga,no huo ni uongo mtupu ni mashabiki wake wa hip hop ndo wanaomuwezesha so anawakanganya wapenzi wake kiukweli.

Sisi kama washikadau wakubwa wa muziki huu wa Ragga na Reggae tumesikitishwa sana kwa mapungufu makubwa ya msanii huyo AY kuzidi kukumbatia ujinga unaofanyika kila mwaka sijui anataka tujifunze nini msanii huyo bwana Ambene yesaya.

Atumchukii AY hapana ila tunajalibu kuweka mambo wazi na kutoruhusu ujinga huu kuendelea maana kunawakati ataimba Taarabu na na Bolingo na watamuweka kwenye category hiyo na atachukuwa.inawezekana kabisa akawa anauwa muziki wake ama anawagawanya mashabiki wake kwa kutotulia kwenye style ya muziki wake,na kuwa kama Inzi anavyotua mara kwenye embe bovu mara kwenye kidonda mara jalalani,atumuelewi bwana A.Y

Tungependa washikadau wa wakubwa wa muziki huu walione kama hili ni tatizo na walikemee kwa nguvu zote ili Tanzania iwe na ukomavu wa muziki huu tofauti na hapo tutakuwa tunapiga kwata bila kusonga mbele.

Sisi tumeshafanya nyimbo kama Heat na Show me some love ambazo zimefanya wema katika vituo mbalimbali lakini tumeenguliwa kwenye tunzo hizo hii inakatisha tamaaaa sana,lakini sisi hatutokata tama na wala haitufundishi uonga wa kupigana na kitu ambacho tunaamini tunakifanya vema kabisa japo kuna wasanii wengi wakali waliamua kuachana na muziki kwa ajiri ya mambo ya kinyama kama haya

Shabiki wetu jaribu kuingia kwenye youtube na usearch Jahson & Susu ama Jahson Tanzania alafu utoe coment je tunastahili kunyimwa tunzo hizo?

Asanteni ni sisi Jahson na Susu

Posted by Unknown on 10:29 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added