|

KILIMANJARO AWARDS YAZUNGUMZA KUHUSU WALIOJITOA KWENYE TUZO HIZO!



Baada ya wasanii kadhaa kutangaza kwamba hawataki kushirikisha kwenye Tuzo za KILI, mmoja kati ya waandaaji wakubwa wa tuzo hizo akiwa amefanya hivyo kwa miaka mitatu mfululizo Ras Inno Nganywagwa ameamplfy kwa upana.
Inno amesema “kwanza kwa mtu anaejitoa kabla ya mechi ni kwamba anaogopa mechi, mara nyingi hawa wasanii wanaelewa kalenda ya Tuzo iko vipi kwa hiyo wanatakiwa kusema kabla, hizo ndio taratibu za kujitoa kwa sababu wamesajiliwa baraza la sanaa la Tanzania”
Akiamplfy zaidi, Inno amesema “lakini pia unajitoa kwa sababu zipi? manake kwa mwaka wa tatu sasa hivi tuzo zimejaribu kuleta mabadiliko fulani, kweli miaka ya nyuma kulikua na kasoro nyingi kwenye tuzo lakini kadri siku zinavyozidi kusonga mabadiliko yanakuepo”
Katika sentensi nyingine Inno amesema ” kuna wengine wanatamka kwamba wamejitoa wakati hata hawakuchaguliwa kushiriki kwenye tuzo za mwaka huu hata kwenye mchakato wa kuwatafuta washiriki wa mwaka huu hawakujadiliwa, huwezi kujitoa kwenye nyumba ambayo hauko ndani yake”
millardayo.com ilipomuuliza Inno kuhusu Dully Sykes ambae yuko kwenye nomination lakini ametangaza hataki kushirikishwa, Inno ameamplfy kwamba “itategemea na itakavyotokea kwa sababu ukisema umejitoa unapunguza nafasi ya kura za mashabiki, nini kitatokea kama mashabiki wakikupa ushindi na kura zao, utakuja kuchukua Tuzo? kwa sababu tuzo unapewa, pesa pia unapewa tofauti na tuzo nyingine za ulaya ambazo huwa fedha hazitolewi, sisi pia tunatoa nafasi ya TOUR ya kuzunguka nchi nzima kwa washindi wote wa tuzo”
Kwa kumalizia, Inno amesema wasanii wengi wa Tanzania wamekua wakikosa nafasi hata za kuwepo kwenye nomination kwa sababu category ni chache tofauti natuzo nyingine kubwa za Ulaya na Marekani ambazo huwa zinakua na Category nyingi kama Grammy yenye 73 tofauti na KTMA ambayo ina category 22 tu.
Wiki moja iliyopita, mwimbaji Dully Sykes na Jaffarai wametangaza hadharani kwamba HAWATAKI kushirikishwa vyovyote kwenye tuzo hizo.

Posted by Unknown on 5:28 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added