|

DUDUBAYA KUIHAMA DAR ES SALAAM MOJA KWA MOJA!


Hii nafasi nimeitoa kwa mshkaji mwenye umri wa miaka 32, mshkaji ambae jina lake la kisanii ni miongoni mwa mwajina yaliyoingia kwenye kitabu cha kumbukumbu cha wakali wa bongo fleva waliowahi kuzishikilia kwa muda mrefu chat za bongo fleva kutokana na hits walizotengeneza.Ni DUDUBAYA anaeishi area 88.4 Dar es salaam, ambae leo ametangaza rasmi kupitia millardayo.com kwamba anajipanga kuihama Dar es Salaam na kwenda kuishi kwao kiseza Mwanza moja kwa moja ndani ya miaka mitatu ijayo, kwa sababu mbili kubwa.Ya kwanza ni joto ambalo limezidi na ya pili ni foleni ambayo huwa inachukua saa kadhaa kufika anakokwenda.Dudubaya ambae alianza maisha ya kujitegemea Dar es salaam miaka saba iliyopita amesema kwa sasa anakaribia kumalizia nyumba yake anayoijenga huko nyumbani kwao Mwanza ambayo imechukua zaidi ya milioni kumi mpaka sasa.amesema “zamani Dar haikua na foleni kubwa hivi, tulikua tunapanda daladala tuna machungu ya kununua gari ili kukwepa foleni na kero za daladala lakini sasa hivi mwenye daladala na mwenye gari wote mko sawa, mnapanga foleni”Sasa hivi Dudubaya ana kampuni inajihusisha na kuuza madirisha na milango ya mbao, pamoja na kampuni ya kuandaa show za wasanii kwenye mikoa mbalimbali ya Tanzania, anacheza movie za kibongo pia

Posted by Bongo Flavor on 7:35 AM. Filed under . You can follow any responses to this entry through the RSS 2.0. Feel free to leave a response

Blog Archive

Labels

Recently Commented

Recently Added